TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

TANZANIA ORGANIC AGRICULTURE MOVEMENT (TOAM) YATANGAZA MKUTANO WA TATU WA KITAIFA WA KILIMO HAI (III- NEOAC)

Dar es Salaam, 12/09/2023 – TOAM, ambaye ni mratibu na mhamasishaji wa sekta ya kilimo hai nchini Tanzania, inafurahi kutangaza Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kilimo Hai. (NEOAC). Mkutano huo utafanyika Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Novemba 2023.

 

NEOAC ni tukio lenye kusubiriwa kwa hamu ambalo linakutanisha wakulima, wanazuoni, watafiti, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, watungasera, na walaji ambao wanapenda mustakabali wa mifumo endelevu ya uzalishaji wa chakula.

Chini ya kaulimbiu “Kutunza vya Asili, Kwa Afya Bora,” NEOAC ya tatu inalenga kuchochea juhudi na mchakato uliopo ili kuhamisha Kilimo Hai cha Ekolojia (EOA) kutoka kwenye majadiliano kwenda kwenye hatua na matokeo katika ngazi ya nchi kwa kutoa jukwaa la kubadilishana habari na uzoefu muhimu, na kujadili masuala ya sera na hatua ambazo zinaweza kusaidia EOA katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

 

Mkutano huo utakuwa na wasemaji maarufu, warsha za kubadilishana uzoefu, majadiliano ya wazi, na vikao vya taarifa. Washiriki watapata fursa ya kushirikiana na wataalamu wa sekta, kuuliza maswali, na kupata ufahamu muhimu katika maendeleo ya hivi karibuni katika kilimo hai. Mkutano pia utatoa jukwaa kwa wakulima kushiriki uzoefu wao, changamoto, na shuhuda za mafanikio, kukuza uelewa na ushirikiano

NEOAC sio tu jukwaa la kubadilishana maarifa na habari, lakini pia ni fursa kwa soko la bidhaa za kilimohai. Washiriki kutoka sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wauzaji wa pembejeo, watengenezaji wa vifaa, wasindikaji wa vyakula na wauzaji, wataonyesha bidhaa zao, hivyo kutoa rasilimali muhimu na fursa za ushirikiano kwa washiriki.

 

Ikiwa wewe ni mkulima mwenye uzoefu katika kilimo hai, mdau unayetaka kuhamia katika mfumo wa kilimo hai, mtafiti, au mtu mwenye nia ya kilimo endelevu, mkutano huu uliopangwa ni fursa sahihi kwako. Mkutano huu utahakikisha kutoa hamasa, elimu, na uwezeshaji kwa watu binafsi ili kuchangia katika mustakabali wenye afya na endelevu zaidi.

USAJILI

Usajili umefunguliwa sasa, na kwa taarifa zaidi kuhusu mkutano, kujisajili, au kutuma andiko la kuwasilisha kwenye mkutano, tafadhali tembelea tovuti ya www.kilimohai.org.

MASWALI

Kwa maswali ya vyombo vya habari, fursa za udhamini, au taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: Brigitha Didas, Meneja wa Programu wa TOAM Mawasiliano: 0652699554 Barua pepe: toam@kilimohai.org

Kuhusu Tanzania Organic Agricultural Movement (TOAM)

TOAM ni shirika lenye wanachama ambalo lihamasisha na kusimamia maendeleo ya kilimo hai nchini Tanzania.

Tunaendelea kufanya kazi kwa bidii kuhamasisha faida za kilimo hai, kuwasaidia wakulima kwa kutoa elimu na ujuzi muhimu, uthibitisho wa mchakato wa uzalishaji wa bidhaa na vituo vya masoko, na kuongeza uelewa kwa watumiaji kuhusu umuhimu wa bidhaa za kilimohai.

 

Kupitia matukio, utafiti, na utetezi, tunajitahidi kuunda mifumo ya uzalishaji wa chakula endelevu na imara kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.